Joy FM

Diwani aomba serikali kutatua changamoto ya barabara

3 October 2024, 13:46

Madiwani wakiwa katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma

Serikali wilayani Kasulu imesema tayari imefanya upembuzi wa baadhi ya barabara ambazo zimekuwa na changamoto ya kutopitika baada ya kuharibika kutokana na mvua za msimu uliopita ili kuweza kutenga bajeti ya kuzifanyia ukarabati.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Kufuatia Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Wilaya ya Kasulu kushindwa kufungua barabara mpya za kata ya Muhunga zinazoelekea maeneo tofauti tofauti Diwani wa kata hiyo Suku Leonard ameiomba serikali kuangalia njia nyingine ambayo inaweza kusaidia kuondoa changamoto hiyo ili kuwepo na urahisi wa kusafirisha bidhaa kwenda maeneo mbali mbali.

Diwani Suku Leonard ametoa ombi hilo wakati akizungumza katika kikao cha robo ya tatu ya mwaka 2023/2024 cha baraza la madiwani wa halamshauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Muhunga Suku Leonard

Kwa upande wake kaimu meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini wilayani Kasulu Mhandisi Erick Raban amekiri uwepo kwa changamoto hiyo.

Sauti ya Kaim Meneja wa wakala wa TARURA Wilaya ya Kasulu

Naye kaimu katibu tawala mkoa wa Kigoma Bi. Jesca Fupi amesema serikali itafanyia kazi changamoto hizo kwa kushirikiana na mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl Vumilia Simbeye.

Katika hatua nyingine amewahimiza madiwani kuhakikisha wanakuwa mabalozi kwa kuwahimiza wananchi kushiriki katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa.

Sauti ya Kaimu Katibu tawala Mkoa Bi. Jesca Fupi