Joy FM

Wananchi wenye sifa watakiwa kugombea nafasi za uongozi Kasulu

30 September 2024, 12:46

Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Picha na Hagai Ruyagila\

Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mji Kasulu ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mwl. Vumilia Simbeye amewataka wananchi kujitokeza na kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu Mji

Wananchi wenye sifa za kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa wialayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kujitokeza kuchukua fomu ili kugombea nafasi hizo.

Akizungumza na Waandishi wa habari, watendaji wa mitaa na kata, wananchi, pamoja na viongozi wa dini Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo amesema zoezi la uchukuaji fomu litaanza rasmi tarehe 1 Novemba 2024.

Sauti ya Msimamizi wa uchaguzi na Mkurugenzi Kasulu TC

Kwa upande wao viongozi wa dini kutoka wilayani Kasulu akiwemo Shekhe Nasibu Rajabu katibu wa jumuiya ya maridhiano wilaya ya Kasulu na Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Mwilamvya Ashely Mageje Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT Kasulu Mjini wamesisitiza kuilinda amani iliyopo na kuzingiatia haki wakati wa uchanguzi utakapofika ili kuepusha vurugu katika jamii.

Sauti ya viongozi wa dini kutoka wilayani Kasulu akiwemo Shekhe Nasibu Rajabu katibu wa jumuiya ya maridhiano wilaya ya Kasulu na Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Mwilamvya Ashely Mageje

Baadhi ya wananchi kutoka halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wamesema ni haki ya kila mtanzania mwenye sifa kuchukua fomu na kugombea nafasi yoyote ya uongozi ili kusimamia na kutekeleza shughuli za kimaendeleo katika jamii.

Sauti ya wananchi kutoka halmashauri ya Mji Kasulu
Baadhi ya wananchi kutoka halmashauri ya Mji Kasulu wakiwa katika kikao na msimamizi wa uchaguzi, Picha na Hagai Ruyagila

Zoezi la uandikishaji wa mpiga kura litafanyika Oktoba 11- 20, 2024 na kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 20 mpaka 26 novemba 2024 huku  uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika tarehe 27 novemba 2024.