Joy FM

Wapanda juu ya miti kutafuta mawasiliano Geita

18 July 2024, 11:40

Mnara wa mawasiliano ukiwa ni miongoni mwa minara 758 inayojengwa nchi nzima, Picha na Samwel Masunzu

Serikali imesema itaendelea kujenga minara nchini nzima ili kuhakikisha mawasiliano yanapatikana kwa wananchi waliokuwa hawapati mawasiliano ili kuchochea maendeleo.

Na Samwel Masunzu

Wananchi wa kata ya Nyakagomba wilayani Geita mkoani Geita wamesema walikuwa wanalazimika kupanda kwenye vichuguu na milima kutafta urahisi wa mtandao kutokana na changamoto iliyokuwepo ya kutokuwa na manara wa simu kwenye eneo lao.

Waziri wa Habari, Mawasliano na Teknolojia ya Habari Nape  Nnauye akikagua minara ya mawasliano, Picha na Samuel Masunzu

Wananchi hao wameeleza hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Mawasliano na Teknolojia ya Habari Nape  Nnauye ya kukagua minara ya mawasliano inayojengwa kwa fedha za ruzuku kutoka serkalini.

Wamesema kwa sasa baada ya mnara kujengwa huduma za mawasliano zimekuwa rafiki.

Sauti ya mkuu wa wilaya Geita

Naye waziri Nape Nnauye amesema mnara huo ambao umegharimu  zaidi ya shilingi milioni 130, hautakuwa na maana kwa wananchi kama hawatautumia vyema.

Sauti ya Naye waziri Nape Nnauye