Joy FM

Maafisa ardhi Kigoma watakiwa kupima maeneo, kutoa hatimiliki

21 June 2024, 12:33

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye, Picha na Mwandishi wetu

Katika kukabiliana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza maeneo mbalimbali nchini, Halmashauri ya wilaya Kasulu kupitia kwa maafisa ardhi kupima maeneo yote na kutoa hatimiliki.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu ametakiwa kuwaagiza maafisa ardhi kupima na kurasimisha maeneo yote yanayoyomilikiwa na Halmashauri hiyo yaweze kupatiwa hatimiliki ili kuepuka migogoro ardhi baina ya wananchi na serikali.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa kigoma kamishina jenerali msitaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye wakati akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la madiwani katika halmashauri hiyo.

Mh.Andengenye amesema baadhi ya migogoro ya ardhi inatokana na kukosekana kwa hatimiliki pamoja na kutokuonekana kwa mipaka inayotenganisha eneo la serikali na eneo la wananchi ambapo ametoa wito wa kupimwa kwa mipaka ikiwa ni pamoja na kutaftiwa hatimiliki  baadhi ya taasisi za shule na vituo vya kutolea huduma za afya.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa kigoma kamishina jenerali msitaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye

Aidha mh.Andengenye ameagiza kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kudhibiti kuvuja kwa mapato pamoja na kufuatilia wadaiwa sugu waweze kulipa madeni ya halmashauri hiyo ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa kigoma kamishina jenerali msitaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye

Akizungumza kwa niaba ya madiwani mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kasulu bw.Elia kagoma amesema wataendelea kushirikiana na halmashauri hiyo kuhakikisha maelekezo yote yaliyotolewa na serikali yanatekelezwa kwa wakati kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Madiwani wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani, Picha na Michael Mpunije