Joy FM

RC Kigoma atoa mwezi mmoja Kasulu kujibu hoja za CAG

20 June 2024, 13:45

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna jenearali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andegenye, Picha na Hagai Ruyagila

Halmashauri ya wilaya kasulu imetakiwa kupitia na kujibu hoja zote zilizoibuliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG ili kuondoa dosari za mahesabu.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna jenearali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andegenye amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu kuhakikisha wanajibu hoja zote za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG walizotakiwa kutolea ufafanuzi ili kuondoa mkanganyiko wa mahesabu uliopo.

Madiwani wakiwa katika baraza la madiwani, Picha na Hagai Ruyagila

Andengenye ameyasema hayo baada ya kusomwa kwa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu taarifa ya hesabu za halmashauri ya wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha ulioishia juni 30, 2023 na miaka ya nyuma inayowasilishwa katika kikao maalum cha baraza la madiwani katika halmashauri hiyo juni 19, mwaka huu.

Amesema zoezi hilo la kujibu hoja liende sambamba na kujibu maagizo matano ya kamati ya bunge ya hesabu za serikali (LAAC) na taarifa ya utekelezaji zipelekwe kwake kabla ya tarehe 1 mwezi agosti mwaka huu.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna jenearali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andegenye

Aidha Andengenye ameitaka halmashauri hiyo kufanya maandalizi mapema ya ukaguzi ujao kwa kutoa ushirikiano kwa mkaguzi wa ndani wa halmashauri ili kubaini changamoto zilizopo wakati huo madiwani wakitakiwa kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa kujibu hoja zote.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna jenearali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andegenye

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amewasisitiza watumishi wa umma kuhakikisha wanafuata maelekezo ya serikali kuliko kufuata maelekezo yao binafsi.

Mkuu wa wilaya wa wilaya kasulu Isac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya mkuu wa wilaya Kasulu kanali Isac Mwakisu

Naye Mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya Kasulu Eliya Kagoma kwa niaba ya madiwani wa halmashauri hiyo amesema wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na serikali ili kuondoa changamoto iliyopo kwenye ripoti ya CAG.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya kasulu

 Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya Kasulu imepata hati safi ya ukaguzi wa mahesabu katika mwaka wa fedha 2022/2023