Joy FM

World vision kusaidia wanafunzi kitaaluma

19 June 2024, 11:59

Ni muonekeno wa baadhi ya miradi inayotekelezwa na world vision kupiti mradi wa buhoma, Picha na Mtandao

Wadau wa maendeleo wilayani kasulu mkoani kigoma wametakiwa kuunga mkoni juhudi za serikali katika kutatua changamoto zinazokabili sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa.

Na Michael Mpunije

Shirika la World vision Tanzania kanda ya Kigoma limesema litaendelea kushirikiana na Serikali kutatua baadhi ya changamoto zilizozopo katika shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu ili kusaidia wanafunzi kufanya vizuri kitaaluma.

Kaimu meneja wa mradi wa Buhoma unao tekelezwa katika kata ya makere kutoka Shirika la World vision Bw. Emmanuel Ntachombonyi amesema wanaendelea na jitihada za kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari.

Bw.Emmanuel amesema shirika hilo limebaini uwepo wa changamoto zilizopo kwenye baadhi ya shule hizo ikiwemo uhaba wa matundu ya vyoo pamoja na uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa hivyo wanashirikiana na serikali kutatua changamoto hizo.

Sauti ya Kaimu meneja wa mradi wa Buhoma unaotekelezwa katika kata ya makere kutoka Shirika la World vision Bw. Emmanuel Ntachombonyi

Katika kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa wanafunzi shirika hilo pia limesema kupitia mradi wa elimu wamefanikiwa kutoa vitabu katika baadhi ya shule za msingi na sekondari pamoja na kuwapatia mavazi ya shule baadhi ya wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.

Sauti ya Kaimu meneja wa mradi wa Buhoma unaotekelezwa katika kata ya makere kutoka Shirika la World vision Bw. Emmanuel Ntachombonyi

Baadhi ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu wameomba wadau wa maendeleo kutatua baadhi ya changamoto zinazowakibili ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama ili kuwakinga na magonjwa ya mlipuko.