Wajasiriamali tumieni vitambulisho kupata mikopo
8 May 2024, 13:13
Serikali imewataka wajariamali kutumia vitambulisho vya ujasiriamali kama sehemu ya kuwawezesha kupata mikopo itakayowasaidia kujiendeleza kibiashara.
Na Hagai Ruyagila – Kasulu
Wajasiriamali wadogo wadogo wa halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuwa na kitambulisho cha ujasiriamali ambacho kitamsaidia kupata mkopo seriakalini na taasisi binafsi ili kufanya maendeleo katika biashara yake.
Hayo yamebainishwa na Afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri ya Mji Kasulu Bi. Rebeka Mpango ambaye ni mratibu wa zoezi la usajiri wa vitamburisho kwa wajasiriamli wadogo wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali hao katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Amesema kwasasa serikali imeboresha kitamburisho hicho cha mjasiriamali na kinafaida kubwa kwake ikiwemo kumsaidia kupata mkopo katika taasisi mbali mbali zilizopo hapa nchini jambo ambalo lisamsaidia mjasiriamali huyo kupata maendeleo yake binafsi na serikali kwa ujumla.
Aidha Bi. Mpango amesema licha ya kupata mikopo kutoka serikalini na taasisi binafsi kupitia kitambulisho hicho pia kitamsaidia kupata msaada pale atakapo kuwa ameibiwa biashara yake.
Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali akiwemo Julius Lameck, Uzia Gabriel na Asifiwe Zaledi wameupongeza uongozi wa halmashauri ya Mji Kasulu kwa namna uvyothamini wajasiriamali hao ili nao watambulike kisheria kupitia biashara zao wanazo zifanya.
Wajasiriamali.Kitambulisho hicho cha mjasiriamali kimeandaliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambacho kitatumiwa na akimama lishe na baba lishe, wasafirishaji ambao ni boda boda na bajaji wamachinga na wauza samaki pamoja na mboga mboga.