Mpanda FM

Recent posts

2 December 2023, 3:41 pm

RC Katavi apiga marufuku shughuli katika hifadhi ya barabara

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Wajumbe katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa Wananchi watakaobainika kufanya Shughuli zilizo kinyume katika hifadhi ya Barabara. Na Anna Milanzi -Katavi Mkuu wa Mkoa wa…

2 December 2023, 1:59 pm

60% ya familia Mpanda zatajwa kutelekezwa na mmoja wa wazazi

Picha na Mtandao Wanaume Wameonekana kuwa na Kiwango Kikubwa cha Utelekezaji wa Familia ikilinganishwa na Wanawake. Na Gladness Richard-Katavi 60% ya Familia Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi zimetajwa kutelekezwa na  Mmoja wa Wazazi huku hali hiyo ikisababisha Watoto kutopata haki…

24 November 2023, 10:34 am

Tanganyika yanufaika na faida ya mauzo ya tumbaku

Uongozi wa Premium Active Tanzania wakikabidhi Mfano wa Hundi yenye Thamani ya Tshs Milion Hamsini na Laki Tatu Kwa Mkuu wa wilaya ya Tanganyika .Picha na Anna Milanzi Wasimamizi wahakikishe wanakabidhi akaunt za kata hizo kwa kampuni hiyo ili mchakato…

22 November 2023, 10:31 am

Zaidi ya watoto 20 huzaliwa njiti kila mwezi mkoani Katavi

Mama anapojihisi kuwa ni mjamzito ni bora awahi kituo cha kutolewa huduma za afya ili kuepuka kujifungua mtoto kabla ya wakati. Na Gladness Richard-Katavi Zaidi ya watoto 20 kila mwezi ndani ya mkoa wa Katavi wameripotiwa kuzaliwa wakiwa njiti huku…

21 November 2023, 10:34 pm

Mbunge Kakoso awakataa madereva walevi

Mbunge Kakoso ameshauri halmashauri hiyo kufanya marekebisho ya magari yaliyoharibika ili yaweze kuendelea kutoa huduma. Na Anna Milanzi -Katavi Mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini mkoani Katavi amekabidhi gari mpya ya wagonjwa  kwa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika huku akisisitiza…

21 November 2023, 8:33 pm

Machinga Katavi walia na kampuni za utoaji mikopo isiyozingatia sheria

Picha na Mtandao Baadhi ya kampuni hizo zinatoa mikopo kwa kutofuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria. Na John Benjamini-Katavi Wafanyabiashara wadogo [machinga]  mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuzifuatilia kampuni ambazo zinajihusisha na utoaji wa mikopo kwa wafanyabiashara kutokana na…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.