Mpanda FM

Wafanyabiashara watakiwa kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko

26 November 2022, 6:56 am

MPANDA

Wafanyabiashara kata ya Kashaulili manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara ikiwa ni pamoja na kuchukuwa tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko.

Wito huo umetolewa na Afisa mtendaji wa Kata ya Kashaulili Merry Ngomarufu amesema kuna baadhi ya wanyabiashara ambao wamekuwa hawashiriki kufanya usafi hususani katika biashara zao na kusisitiza wafanyabiashara wote kuendelea kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kwa kuweka maji tiririka katika biashara zao.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wamewakumbusha wafanyabiashara wenzao kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara pamoja na kuwa na vifaa vya maji tiririka kwa ajili ya kunawa mikono ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.