Mpanda FM

Mkuu wa Wilaya: Wakurugenzi Simamieni Miradi

20/11/2021, 12:30 PM

Mkuu wa wilaya ya  mpanda Jamila Yusuph amewaagiza wakurugenzi wa manispaa ya  mpanda na halmashauri ya nsimbo  kusimamia miradi ya maendeleo ili inapokamilika iwe na ubora unaoendana na thamani ya pesa iliyotolewa.

Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya (DDC) katika ukumbi wa manispaa amewataka wakurugenzi kuwasimamia wataalamu wanaofanya  miradi ya maendeleo kuhakikisha inakuwa katika ubora unaotakiwa.

Kwa upande wake mbunge wa mpanda mjini Sebastian Kapufi amesema sio mbaya kutumia wataalamu wa ndani ila ni lazima kuzingatia ubora na uwezo wa mtaalamu katika utendaji kazi.

Miradi mingi ya kimaendeleo imekuwa ikisuasua, kutokana na baadhi ya wakandarasi kutokuwa na utaalamu wa kutosha, katika utekeleza wa miradi hiyo.