Mpanda FM

Maoni ya Wananchi juu ya Katazo kwa Madalali

20/11/2021, 1:06 PM

Baadhi ya wananchi manispaa ya mpanda  mkoani katavi wamekuwa na maoni tofauti juu ya katazo la madalali wa nyumba  kupewa kodi ya mwezi mmoja.

wakizungumza na mpanda  radio fm wananchi hao wameleza kufurahishwa kwa marufuku hiyo huku wengine wakionesha kutoridhishwa na maamuzi hayo.

Sauti za Wadau

kwa upande wake israeli mwaipopo ambae ni dalali wa nyumba ameeleza moja ya changamoto wanayokutana nayo ni wamiliki wa nyumba kutokukubali kulipa asilimia kumi ya kodi wanayopangisha hali inayowapelekea kuomba pesa hiyo kutoka kwa wapangaji.

Sauti ya Dalali

Hivi karibuni waziri wa  Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepiga marufuku kwa madalali wa nyumba  wanaochukua kodi ya mwezi mmoja kwa wapangaji kuacha tabia hiyo na badala yake pesa hizo zilipwe na wenye nyumba.