Mpanda FM

Madereva Zingatieni Sheria za Barabarani

20 November 2021, 10:52 am

Madereva wa vyombo vya moto mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria na taratibu zote za usalama barabarani.

Wito huo umetolewa mapema leo na Sanjeti Jofrey Britoni wakati akizungumza na kituo hiki na kubainisha kumekuwa na madereva wanaovunja na kukaidi kufuata utaratibu wa sheria za usalama barabarani.

Sauti ya Sajenti

Katika kuhakikisha wanadhibiti mwendo kasi kwa madereva wa vyombo vya moto Sajenti Jofrey amesema kwasasa umewekwa mfumo wa kudhibiti mwendo kasi kwenye magari makubwa ya abiria.

Hata hivyo amewataka madereva wa magari ya serikali kuzingatia sheria za usalama barabarani huku akiahidi hatua stahiki zitachukuliwa kwa yeyote anaebainika kuvunja sheria za usalama barabarani.