Mpanda FM

Wafanyabiashara Soko la Matunda Walia na Vibanda

19/11/2021, 10:44 AM

Baadhi ya wafanyabiashara soko la matunda lililopo mtaa wa kawajense Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameuomba uongozi wa soko kuwawekea mfumo mzuri wa uwepo wa vibanda vya kuuzia bidhaa zao.

Wakizungumza na mpanda radio FM wafanyabiashara hao wamezitaja changamoto zinazowakabili katika soko hilo ikiwa ni pamoja na miundombinu mibovu.

Sauti za Wafanyabiashara

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko la matunda Isaka marko amekiri kuwepo kwa changamoto zilizopo katika soko hilo na kuishauri serikali kubadili mfumo wa soko ili kuweza kukaa katika mpangilio mzuri.

Sauti ya Mwenyekiti wa Soko la Matunda