Mpanda FM

Million 245 za Mkopo wa Asilimia Kumi Katavi

19 November 2021, 12:12 pm

Zaidi ya shilingi milioni mia mbili arobaini na tano zimetolewa  kwa wanawake vijana na watu wenye ulemavu ambao ni wanuafaika wa mkopo wa asilimia kumi kutoka manispa ya mpanda mkoani katavi.

Akikabidhi mikopo hiyo katika ukumbi wa manispaa mkoani katavi Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewataka wanufaika kutumia pesa hizo kwa malengo waliosainia katika mikataba na halmashauri na siyo katika matumizi yao binafsi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Mpanda

Aidha Mstahiki meya wa manispaa ya mpanda Aidari sumri ameeleza kuwa mikopo hiyo imetolewa bila riba yoyote huku akiwataka wanufaika kutoa taarifa endapo wataombwa pesa ya ziada .

Sauti ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda

Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali kwa kuwapatia mikopo huku wakiahidi kurejesha kwa wakati uliopangwa.

Sauti za Wanufaika

Mkopo wa asilimia kumi katika manispaa ya mpanda umetolewa kwa vikundi arobaini na  saba  huku wanawake wakiwa 38 vijana 7 na watu wenye ulemavu 2