Joy FM

Wananchi watakiwa kushiriki katika utekelezaji miradi ya maendeleo.

8 January 2025, 11:25

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina,-Picha na Tadio

Ushiriki wa mwananchi mmoj mmoja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kunasaidia miradi kukamilika kwa wakati ili kukamilisha kwa wakati.

Na Michael Mpunije – Buhigwe

Wananchi wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wametakiwa kushirikiana na Serikali kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina ambapo ameeleza kuwa ni jukumu la wananchi kushirikiana na Viongozi wa Halmshauri katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na kukamilika kwa Wakati.

Kanali Ngayalina amesema serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali  za wananchi ikiwemo miundombinu ya barabara na maji.

Suti ya Mkuu wa wilya ya Buhigwe Kanali Ngayalina

Aidha Kanali Ngayalina Amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia fursa zilizopo katika vijiji vyao na kuongeza bidii katika shughuli za Kilimo ili kuleta maendeleo kwenye jamii.

Sauti ya mkuu wa Wilya ya Buhigwe.