Joy FM

Tanzania, Burundi kuimarisha usalama mipakani

16 December 2024, 12:53

Pichani ni viongoz wa mkoa wa Kigoma wakiwa na viongozi mbalimbali toka Nchini Burundi katika maadhimisho ya miaka 20 ya ujirani mwema,- Picha na Josephine Kiravu

Uimara wa hali ya usalama wa mipaka ya Tanzania na Burundi utaimarisha uchumi na shughuli za Kibiashara.

Na Josephine Kiraavu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaaf wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengnye amesema Serikali itaendelea kutekeleza maazimio ya ujirani mwema yaliyoanzishwa hapo awali huku akisisitiza usimamizi wa usalama maeneo ya mpakani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 20 ya ujirani mwema kati ya mkoa wa Kigoma na mikoa 6 ya Burundi amesema kwa sasa hali ya usalama inaimarika na vikao hivi vianendelea kujadili mahusiano hasa ya kiusalama, kiuchumi na kuimarisha biashara maeneno ya mipakani.

Sauti ya Mkuu wa Kigoma

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Makamba ambae pia ni mwenyekiti wa ujirani mwema Burundi Tantine Ncutinamagara ameshukuru uwepo wa vikao vya ujirani mwema na kwamba utaleta mabadiliko makubwa si kwenye masuala ya usalama pekee bali hata kwenye biashara.

Sauti ya mkuu wa Mkoa wa Makamba Nchini Burundi

Nao waasis wa ujirani mwema akiwemo Katibu mkuu wa chama tawala nchini humo Reverien Ndikuriyo na Mkuu wa mkoa wa kigoma mstaafu Kanali Elmon Mahawa wamesema vikao hivi vya ujirani mwema vilianza rasmi mwaka 2004 kufuatia kukosekana kwa hali ya usalama nchini Burundi na matarajio yao kwa sasa ni kuona vikao hivi vinaleta manufaa kwenye masuala ya biashara.

Sauti za waasisi wa ujirani mwema kati ya Kigoma na Mikoa sita ya Burundi

Kikao cha ujirani mwema kimejadili maswala mbalimbali ikiwemo maboresho ya pasi ya ujirani mwema kwa kuiongeza muda wa matumizi kutoka siku 14 hadi miezi 3.