Joy FM

Kamati vyama vya siasa yaridhishwa mwenendo wa uandikishaji

24 October 2024, 12:14

Mwenyekiti wa kamati maalumu ya Umoja wa vyama vya siasa mkoani Kigoma, Picha na Josephine Kiravu

Viongozi wa siasa mkoani Kigoma kupitia Umoja wa vyama vya siasa mkoani hapa wameeleza kuridhishwa na zoezi la uandikishaji kwenye daftari la wakazi kwa ajili ya kupata sifa ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba 27,2024.

Na, Josephine Kiravu

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati maalum ambayo iliundwa kwa lengo la kutembelea halmashauri za mkoa ikiwemo Kigoma Manispaa,Kigoma DC, Kasulu TC, Kasulu DC,pamoja na Buhigwe ili kujionea hali ilivyo kufuatia kuzuka kwa taarifa zinazoeleza mwitikio hasi wa wananchi kwenye zoezi hilo.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati maalum ambayo iliundwa kwa lengo la kutembelea halmashauri za mkoa

Kwa upande wake katibu wa kamati hiyo Rajabu Nyambaro ambaye pia ni katibu wa chama cha NCCR Mageuzi amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwenye zoezi hilo huku akiwataka makatibu wa vyama vya siasa kuendelea kuhubiri siasa ambazo hazitaleta uvunjifu wa amani.

Sauti ya katibu wa kamati Rajabu Nyambaro ambaye pia ni katibu wa chama cha NCCR Mageuzi

Kwa upande wao wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Musa Habibbu katibu wa Ada tadea na Amani Salum katibu wa AFP wamesema wameridhishwa na mchakato mzima kwenye zoezi la uandikishaji na kuwataka wakazi waliojiandikisha kutumia haki yao ya kikatiba muda utakapowadia kumchagua kiongozi bora atakaewasilisha vyema changamoto zao.

Sauti ya wajumbe wa kamati

Zoezi la uandikishaji wakazi kwenye daftari la mkazi lilianza Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu ambapo wakazi ambao wamefikisha umri wa zaidi ya miaka 18 wamepata fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 27 mwaka huu

Viongozi wa vyama vya siasa mkoani Kigoma kupitia Umoja wa vyama vya siasa ,Picha na Josephine Kiravu