Wakandarasi REA wanyoshewa kidole Kigoma
20 September 2024, 08:58
Bodi ya Nishati Vijijini REB, imewaonya wakandarasi wanaosuasua kukamilisha miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini REA, ikisisitiza miradi ikamilike kwa wakati katika vijiji vyote vinavyotekeleza miradi nchini, na kusaidia wananchi kupata nishati ya umeme kwa wakati.
REB imezuru miradi inayotekelezwa mkoani Kigoma, katika wilaya za Uvinza na Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo wananchi wameeleza tija ya miradi hiyo na kuomba ikamilike kwa wakati.
Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Saidy amesema vijiji 92 vinaenda kupata nishati ya umeme na kumaliza vijiji vyote 306 kuwa na nishati hiyo kwa mkoa wa Kigoma, wakati Mwenyekiti wa Bodi, Bodi ya nishati Vijijini Barozi Meja Jeneral mstaafu Jacobu Kingu akisisitiza wakandarasi kutekeleza miradi kulingana na makubaliano ya mikataba.