Joy FM

Serikali yaonya upotoshaji zoezi la wakimbizi kurejea Burundi

24 June 2024, 15:35

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Sudi Mwakibasi, Picha na Kadislaus Ezekiel

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeyaonya mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia wakimbizi na kuyataka kutojihusisha na upotoshaji wa kukwamisha zoezi la kuwarudisha wakimbizi wa nchi ya Burundi kwa kuhofia kukosa kazi zao baada ya kufungwa kambi za Nduta na Nyarugusu upande wa wakimbizi wa Burundi ifikapo Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Sudi Mwakibasi amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkimbizi Duniani, ambayo yamefana katika kambi ya eakimbizi Nduta wilayani Kibondo.

Sauti ya Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa Wakimbizi Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi Sudi Mwakibasi

Awali wakieleza juu ya changamoto wanazokabiliana nazo viongozi wa wakimbini katika kambi za Nduta na Nyarugusu wameomba UNHCR kusaidia  nishati safi ya kupikia na huduma za kijamii hasa upande wa matibabu.

Sauti za viongozi wa kambi za wakimbizi nduta na nyarugusu

Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Mahoua Parums amesema shirika hilo litaendelea kutoa misaada ya kiutu na kujali wakimbizi kwa kushirikina na serikali pamoja na wafadhili wengine.

Sauti ya Mwakilishi mkazi wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Mahoua Parums