Wakulima wa kahawa walia na ukosefu wa viwatilifu kakonko
18 April 2024, 14:02
Licha ya elimu ya namna ya kulima kilimo chenye tija kwa wakulima walio wengi nchini lakini bado kilio cha wakulima ni kuona serikali inaboresha upatikanaji wa pembejeo za kilimo.
Na James Jovin, Kigoma
Wakulima wa Zao la Kahawa Wilayani Kakonko Mkoa wa Kigoma wanakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na Pembejeo za Kilimo, Viwatilifu na elimu bora ya Kilimo hicho.
Baadhi ya wakulima Katika Kata ya Lugenge wilayani Kakonko wamesema kutokana na zao hilo kuwa geni kwao bado wanahitaji elimu zaidi ya kilimo hicho lakini pia wameiomba serikali kusaidia kufikisha Pembejeo kwa wakati ili kuepuka hasara.
Kwa upande wake Faustin John Afisa Kilimo Wilaya ya Kakonko amesema idara ya kilimo imejipanga kusaidia Wakulima hao hasa kuwaunganisha na Vyama vya ushirika ili waweze kukopa Viatilifu huku Deusdedit Kilombo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Nchini amesema wamekuwa wakitoa Mbegu ambazo zinavumilia Magonjwa na kuhamasisha wadau kutoa pembejeo kwa wakati
Aidha mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania bw. Kilombo aliendelea kusema kuwa Licha ya Changamoto zilizopo Taasisi yake imekuwa ikijitaidi kuzitatua na kueleza kwa sasa uzalishaji umeongezeka tofauti na miaka ya nyuma ambapo miaka miatu iliyopita walizalisha Tani 50,000 na mwaka jana 2023 walizalisha tani 80,000.
Katika Wilaya ya Kakonko hadi sasa kuna wakulima wa zao la Kahawa wapatao elfu nane tu huku ikikadiliwa kuwa kufikia mwaka 2027 wakulima wa kahawa katika wilaya hiyo watakuwa zaidi ya elfu kumi na tano watakaoweza kuzalisha kahawa zaidi ya tani laki mbili kila mwaka.