Mpanda FM

Sauti ya Katavi (Matukio)

18 May 2023, 7:09 pm

TANGANYIKA.

Wakazi wa kijiji cha kasinde kata ya kabungu Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wameutaka uongozi wa kata hiyo kutatua changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara na madaraja ambayo imekuwa kikwazo kwa kipindi kirefu.

Wakizungumza na Mpanda redio fm wananchi hao wamesema kuwa ubovu wa miundombinu ya barabara imekuwa adha kwao hasa katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

MWANAHABARI WETU BEN GADAU KUTOKA KIJIJI CHA KASINDE ANAOUNDANI WA HABARI HII.

KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema Mkoa utaunda kamati ya kuchunguza tukio la moto ulioteketeza Jengo la Mahakama ya Mwanzo ya Shanwe iliyopo Manispaa ya Mpanda.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kupokea taarifa ya Awali Mrindoko amesema kuwa kamati itafanya kazi kwa siku Tano na inaanza kazi hiii leo.

Mwandishi wetu Henry Mwakifuna asubuhi ya leo amefika kata ya shanwe na kutuandalia Taarifa hiyo.

KATAVI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvu Hoza Mrindoko amefanya ziara ya  kutembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu ya msingi kupitia  mradi wa boost ndani ya kata ya kawajense na kazima.

Miradi ya ujenzi wa miundombinu  ya elimu ya msingi kupitia mradi wa boost hadi kukamilika utaondoa changamoto ya vyumba vya madarasa,vyoo,vichomea taka na nyumba za walimu.Na mwandishi wetu GLADNESS RICHARD ametuandalia undani wa taarifa hiyo.

DODOMA

Baadhi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania wameitaka serikali kuyachukulia hatua mashirika  binafsi na watu wengine wanaoshiriki katika vitendo ya  vya uvunjifu  wa maadili ikiwa ni Pamoja na kuweka sheria  ili kudhibiti  vitendo hivyo.

Hayo yamebainishwa na wabunge wakati wa vikao vya bunge vinavyoendelea jijini dododma ambapo wabunge hao wameonyshwa kukerwa na matendo ambayo yanaenelea kutokea kutoka chumba cha Habari VERONICA MABWILE.

KIGOMA

Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua Opereseheni [+255] yenye lengo la kutoa hamasa kwa Wananchi kukiunga mkono katika harakati.

Operesheni hiyo imezinduliwa mkoani Kigoma na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe Na makamu mwenyekiti Tundu lisu .

 BETORD BENJAMIN KUTOKA CHUMBA CHA HABARI ANAKULETEA TAARIFA HII.

MICHEZO

Wazazi Katavi wameombwa kuwapa nafasi Watoto wao kushiriki katika michezo, Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia suluhu Hassan aongeza pesa kwa yanga katika hatua ya fainali kimataifa Europa leage kuchezwa leo.

Kilian Samwel anakuja na undani wa taarifa hizo za michezo.