Mpanda FM

Wakulima Washukuru kwa Mbolea ya Ruzuku

11 October 2022, 10:35 am

MPANDA

Baadhi ya wakulima wa mazao kata ya Minsukumilo halmashauri ya Mpanda wameishukuru serikali kwa kuwapa ruzuku ya mbolea.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wakulima hao wamesema ruzuku hiyo itasaidia kuongeza mavuno tofauti na hapo awali huku wakiwahamasisha wakulima wengine kuendelea kujiandikisha ili kunufaika na ruzuku hiyo.

Mussa Kiteka ni afisa mtendaji wa kata ya Minsukumilo amesema zoezi la uandikishaji wa mbolea za ruzuku kwa wakulima bado linaendelea huku akiwaomba wakulima kujiandikisha kwa wingi kabla ya ukomo wa zoezi hilo.

Katika siku ya wakulima waziri wa kilimo Hussein Bashe akiwa mkoani Mbeya alitangaza bei mpya ya ruzuku  na ambayo itatumika katika maduka ya pembejeo nchi nzima  na ilianza  rasimi tarehe 15 mwezi wa nane  mwaka huu.