Mpanda FM

TAKUKURU: WANANCHI TUSHIRIKIANE KUTOMEZA RUSHWA

25/05/2022, 4:23 PM

Jamii mkoani katavi imeaswa kushirikiana na tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuku  katika kutokomeza  vitendo vyote vya rushwa mkoani hapa.

Wito huo umetolewa na  Mkuu wa Takukuru Mkoani katavi Festo Mdede wakati akitoa taarifa  ya utendaji kazi wa ofisi ya takukuru kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia January hadi March Mwaka huu.

Aidha mdede ameeleza kuwa kuna wimbi la matapeli  wanaojitambulisha kam mafisa wa takukuru na kuwa pigia watu simu   kwa ajili ya kujipatia fedha hivyo ameomba wananchi kutoa taarifa kwa ofisi ya takukuru wanapokutana na watu wa namna hiyo.

Katika hatua nyingine mkuu huyo amesema wamefuatilia  utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari  na vituo shikizi  na kubaini ubadhirifu wa miradi hiyo hivyo  kuwataka waliotengeneza samani chini ya kiango warudie kwa gharama zao binasi na  wakihakikisha mafundi waliomaliza kazi wanalipwa.