Mpanda FM

MAADHIMISHO YA SIKU YA NYUKI KATAVI

23/05/2022, 2:12 PM

KATAVI

Kufatia maadhimisho ya siku ya nyuki duniani mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka watanzania kutunza mazingira kwa kuhifadhi misitu ili kuongeza thamani ya mazao ya mdudu nyuki.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya nyuki duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani katavi mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mwanamvua Mrindoko amewataka watanzania kutunza misitu ili Tanzania iendelee kunufaika  na mazao yatokanayo na mdudu  nyuki.

Akitoa salamu kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya  mpanda mkuu wa wilaya hiyo Jamila Yusuph ameeleza namna maadhimisho hayo ya siku ya nyuki duniani ambavyo yatawanufaisha wananchi wa wilaya ya  mpanda ikiwemo kujiongezea kipato kwa kuongeza uzalishaji  wa mazao yatokanayo na mdudu nyuki.

Maadhimisho ya siku ya nyuki duniani kwa mwaka huu  yamebebwa na kauli mbiu isemayo  ni nyuki wamehusika harakati za kujikwamua upya zisisahau nyuki.