Mpanda FM

Hifadhi ya Katavi na Utajiri wa Viboko

20/11/2021, 12:25 PM

Hifadhi ya taifa mkoani katavi inatajwa kuwa moja ya hifadhi inayoongoza kuwa na  viboko wengi afrika huku idadi ya viboko hao  ikikadiriwa kuwa ni zaid ya milioni mbili .

Hayo yamebainishwa na muongoza watalii katika hifadhi hiyo God listern Isaya katika  ziara ya waandishi wa habari mkoani humo  iliyoandaliwa na mbunge wa mpanda mjini sebastian kapufi na kueleza kuwa  uwepo wa viboko hao umeifanya hifadhi hiyo izidi kutambulika afrika.

Sauti ya Muongoza Watalii

Aidha  mbunge wa mpanda mjini Sebastian Kapufi amewasisitiza   waandishi wa habari  kuendelea kuitangaza hifadhi hiyo huku akiwataja waandishi hao kuwa ni moja ya makundi yanayosikilizwa katika jamii.

Sauti ya Mbunge wa Mpanda Mjini

baadhi ya waandishi  wameomba mamlaka kuendelea kutangaza utalii wandani ili utambulike zaidi  na hatimae kukuza uchumi wa mkoa na taifa kiujumla.

Sauti za Waandishi

Hifadhi ya taifa ya katavi   mbali kuwa  ni hifadhi yenye viboko wengi afrika bali ni hifadhi pekee duniani anayopatikana twika mweupe.