Mpanda FM

TAKUKURU yabaini mapungufu wilaya ya Tanganyika

26 May 2023, 10:47 am

KATAVI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi imebaini kuwepo kwa mapungufu yakiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa miradi, ukiukwaji wa mikataba na ucheleweshaji wa kukamilisha miradi mitano katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani hapa.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Faustine Maijo amesema miradi iliyokutwa na mapungufu hayo ni ujenzi wa vyumba za walimu shule ya msingi Lwega katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wenye thamani ya mil. 97 ambapo uchuguzi umebaini kuwa kuna ukiukwaji wa taratibu za mkataba na kujenga kinyume na kiwango ilivyoainishwa kwenye mkataba.

Aidha Maijo amesema wamebaini mapugufu katika ujenzi wa mabweni na maabara katika shule ya sekondari Kakoso halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wenye jumla ya thamani ya mil. 300 ambapo kwenye ujenzi wa mabweni wamebaini usimamizi mbovu, ucheleweshwaji wa fedha na mradi wa maabara kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu za mkataba kwa kujenga chini ya kiwango.

Amebainisha kuwa TAKUKURU imeendelea kufanya chambuzi za mifumo ikiwa na lengo la kubaini mianya ya rushwa ambayo inaweza kupelekea vitendo vya rushwa na kushauri taasisi husika kuona namna bora ya kurekebisha mapungufu yaliyobainika kwenye mifumo.

#mpandaradiofm97.0

#TAKUKURU

#Tanganyikadc