Mpanda FM

TAKUKURU yafichua maduka yanayouza viuatilifu mali ya serikali

23 May 2023, 7:32 pm

KATAVI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi imefanikiwa kufichua maduka yanayouza viuatilifu ambavyo ni mali ya serikali chini ya usimamizi wa bodi ya pamba.

Hayo yamesemwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Faustine Maijo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU katika robo ya Januari hadi Machi 2023 mbele ya waandishi wa habari amesema maduka matano (5) yamebainika yanauza viuatilifu aina ya Bodigadi 500 wdg ambavyo ni mali ya serikali.

Aidha Maijo amesema TAKUKURU mkoa wa Katavi imefuatilia utekelezaji wa miradi 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.591 katika sekta za Ujenzi, Elimu na Afya katika ufuatiliaji huo miradi 2 imekamilika, miradi 2 inaendelea vizuri na miradi 5 imekutwa na mapungufu.

Maijo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Katavi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa pindi wanapobaini vitendo hivyo.

#mpandaradiofm97.0

#takukuru