Mpanda FM

Wananchi Kata ya Nsemulwa Walia na Barabara

29 March 2023, 8:29 am

MPANDA

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nsemlwa Halmashuri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba serikali kutengeneza miundombivu mibovu ya barabara iliyopo katika kata hiyo katika kipindi hiki cha mvua za masika ili kuwaondolea adha wanayokutana nayo.

Wakizungumza na kituo hiki wana nchi hao wamesema kuwa hali ya Barabara katika kata hiyo kwa sasa sio rafiki kutokana na baadhi ya maeneo kutopitika kwa sababu za kuchimbuliwa na maji huku wakiyaainisha maeneo ambayo ni mambovu zaidi kuwa ni kichangani pamoja na mtaa wa Migazini.

Kwaupande wake diwani wa kata hiyo Mohamed Bakari Kapona amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa kata hiyo bado inachangamoto kubwa ya miundombinu ya barabara ambapo ameiomba mamlaka ya usimamizi wa barabara Tarura kutumia mfuko wa dharura kuzitengeneza barabara hizo.