Mpanda FM

Mwenyekiti Katumba Aomba Msaada Kukamilisha Ujenzi wa Darasa

29 March 2023, 8:16 am

NSIMBO

Mwenyekiti wa kijiji cha Katumba Salumoni Jeremeiah Mayangu amewaomba wadau na serikali kuwasaidia kukamilisha Ujenzi wa Boma la darasa wa shule ya Msingi Katumba lililoanzwa kujengwa kwa nguvu za wananchi.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa kilele cha wiki ya maji kilichofanyika katika Kijiji hicho Mayangu amesema wananchi wamechangia kiasi cha shilingi elfu 38 kila mmoja ili kuanza kwa ujenzi wa boma ingawa wamekumbwa na mkwamo wa kuchangishana ili kukamilisha ujenzi wa boma hilo.

Akijibu hoja hiyo makamu mwenyekiti wa halmashauri Ya Nsimbo Leam Chalamila amewashukuru wananchi kwa kuanza ujenzi na kuwataka wananchi kufikisha hatua ya lenta ili serikali kupitia halmashauri italeta pesa kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo hilo.

Aidha Chalamila ameongeza kwa kusema kwa mwaka wa fedha unaotarajiwa kuanza 2023/2024halmashauri ya Nsimbo imepanga kujenga maboma 500 ya shule.