Mpanda FM

Waumini wa Dini ya Kiislamu Waaswa Kutenda Mema

27 March 2023, 5:29 pm

KATAVI.

Waumini wa dini ya kiislam mkoani Katavi wameaswa kuachana na mambo yasiyofaa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani na badala yake kuishi kwa wema na kufanya matendo ya kumpendeza mwenyezi mungu na jamii kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na shekh mkuu wa mkoa wa Katavi Mashaka Nassor Kakulukulu ofisini kwake na kusema kuwa mwezi wa ramadhani ni mwezi wa toba hivyo ni muhimu kwa waislamu wote kufunga ili kurejea yaliyo mema mbele ya mwenyezi Mungu.

Nae katibu wa baraza kuu la waislam Tanzania ( BAKWATA) mkoa wa Katavi Omary Ally Muna amewaomba waislam kuendeleza yaliyo mema ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani na baada ya ramadhani huku akiwasisitiza kuishi kwa amani upendo na kusaidiana.

Mwezi mtukufu wa ramadhani unawaunganisha pamoja waumini wa dini ya kiislam kote duniani kwaajili ya toba na kuishi yaliyo mema mbele ya mwenyezi Mungu