Mpanda FM

Diwani Magamba Alia na Tanesco

22 February 2023, 6:24 pm

MPANDA

Diwani wa Kata ya Magamba Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Fortunatus Maiko ameliomba Shirika La Umeme [Tanesco] kutoa ufafanuzi kuhusiana na Matumizi ya unit za umeme ili kuondoa mkanganyiko unaoendelea kuonekana kwa ya wananchi.

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye baraza la madiwani wa Manispaa ya Mpanda na kuhoji kuwa kwa nini unit za umeme zinatofautiana kwenye manunuzi kwa wananchi.

Kwa upande wake Injinia wa mipango Mkoa wa Katavi kutoka shirika la umeme Tanesco Charles Faustine amesema kuwa madaraja ya wateja yanatofautiana kutokana na matumizi ya umeme.

Aidha Injinia Faustine Amesema kuwa mtu ambae hajatumia unit 75 kwa mwezi ndio mwenye sifa ya kuwa daraja zero.