Mpanda FM

Baraza la Kata Litumike Kutatua Migogoro ya Ardhi

10 February 2023, 12:34 pm

MPANDA

Wananchi wa manispaa ya mpanda mkoani katavi Wameshauliwa kutumia baraza la kata kusuluhisha migogoro ya ardhi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi mkoa wa katavi Gregory Rugalema amesema kuwa kupitia mabaraza ya ardhi ya wilaya na kata migogoro mingi imetatuliwa.

Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa ni bora kupeleka migogoro yao ya ardhi kwenye mabalaza ya kata kuliko kukurupuka kwenda ngazi za juu zaidi.

Hata hivyo wananchi wameomba wasimamizi wa mabaraza ya kata ya ardhi kusuruhisha kwa haki na usawa pindi kesi za migogoro ya ardhi zinapojitokeza.