Mpanda FM

Fahamu Matumizi Sahihi ya Alama za Zebra

21 January 2023, 8:34 pm

MPANDA
Madereva wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya vivuko vya barabara ili kuepusha ajali ambazo zinatokea katika vivuko .

Hayo yamesemwa na mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Geofrey Braiton, kuwa ni sheria kwa mtu anaeendesha chombo cha moto kuhakikisha anasimaama pale anapofika katika eneo la kivuko cha watembea kwa miguu au kupunguza mwendo na kujiridhisha pande zote mbili hakuna watembea kwa miguu ndipo aweze kuendelea na safari.

Kwa upande wa waendeshaji wa vyombo vya moto wamesema kuwa wapo baadhi ya madereva ambao hawazingatii sheria ya kusimama au kupunguza mwendo maeneo ya vivuko hususani madereva bodaboda, ambao wamekuwa na tabia za kupita bila kujali vivuko, na wamekuwa wakisababisha kutokea kwa ajali.

Watembea kwa miguu wamesema kuwa ni muhimu kuhakikisha unaangalia na kujiridhisha kuwa chombo cha moto kimesimama, ndipo uweze kuvuka kwani wapo madereva amabo wamekuwa na hali ya kutozingatia vivuko hivyo.