Mpanda FM

Kukosekana Kwa gari ya kuzolea taka kata ya Nsemlwa ni chanzo cha taka kutupwa kwenye mitaro

23/11/2022, 6:19 PM

NSEMLWA
Imeelezwa kuwa kukosekana kwa gari la kuzolea taka katika kata ya Nsemlwa Halmashauri Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi kunachangia baadhi ya wanchi kutupa takataka kwenye mitaro ya kupitishia maji.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakati Wakizumnguza na Mpanda Radio fm ambapo wamesema kuwa hali ya uzoaji wa taka hauridhishi jambo ambalo ni changamoto hasa nyakati za masika .

Diwani wa kata hiyo Bakari Mohamed Kapona amesema hali ya uzoaji wa taka katika kata hiyo umedhorota kutokana na baadhi ya maeneo kutofikika kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara .

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sofia Kumbuli amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa inasababishwa na uhaba wa magari ya kuzolea taka.