Mpanda FM

Wananchi Wadai Fidia Waweze Kuondoka

08/09/2022, 7:27 PM

KATAVI
Baadhi ya wananchi wanao ishi mtaa wa Tambukareli kata ya uwanja wa ndege manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwalipa fidia ili waweze kutoka katika makazi hayo.

Wakizungumza na mpanda redio fm wamesema kuwa ni muda mrefu sasa hawajalipwa ili waweze kutoka katika eneo hilo kitu kinacho wafanya kuendelea kubaki huku wakihatarisha maisha yao.
.
Kwaupande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa katavi Martini Mwakabende amesema kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2007 iliongezwa upana kutoka mita 45-60upande wakulia mita saba na nusu na upande wa kushoto ikiwa ni barabara zote nchini.
.
Mwakabende amewataka watumiaji wote wa barabara kusaidia kulinda miundo mbinu ya barabara kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika miundo mbinu hiyo.