Mpanda FM

CCM Yasafisha Kichaka cha Muda Mrefu

07/09/2022, 10:50 AM

MPANDA

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Mpanda Hotel wameeleza umuhimu wa kufanya usafi wa mazingira.

Wameyasema hayo wakati wakitekeleza zoezi la usafi katika eneo la chama hicho ambalo lilikuwa likitumika kama kichaka cha kutupa taka na wakazi wa karibu na eneo hilo.

Benedict Matimba ni katibu wa chama cha Mapinduzi kata ya Mpanda hotel amesema zoezi la usafi katika eneo hilo linaenda sambamba na uendelezaji wa eneo hilo ambapo kwa sasa chama hicho kinatarajia kujenga vibanda vya biashara pamoja na ofisi za chama.