Mpanda FM

ULEGA: TUMIENI MAFUNDISHO KULETA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA MAZIWA NCHINI

08/06/2022, 3:34 PM

Naibu waziri wa kilimo na uvuvi Abdala Ulega Amezitaka jamii mkoani Katavi kutumia mafundisho waliyoyapata katika maadhimisho ya wiki ya maziwa ili kuleta mabadiliko katika sekta ya maziwa nchini.

Akizungumza wakati wa kufunga wiki ya maziwa mkoani hapa Ulega amesema kuwa serikali imewekeza pesa kwa mwaka wa pesa 2022/2023 katika sekta ya maziwa ambapo million 120 zitatumika kuanzisha kituo cha ukusanyaji maziwa katika manispaa ya  mpanda .

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua hoza mrindoko amewataka  wananchi wa katavi kutumia fursa zilizojitokeza katika maadhimisho katika kukuza uchumi wa wafugaji pamoja na uchumi wa mkoa .

Maadhimisho  ya 25 ya  wiki ya ya Maziwa kitaifa yamefungwa june 1 mkoani hapa na naibu waziri wa kilimo na uvuvi abdala ulega huku yakiwa na  kaulimbiu isemayo  Kunywa Maziwa yaliyosindikwa Tanzania , lishe bora na salama.