Mpanda FM

MIGOGORO NA ATHARI KATIKA NDOA

8 June 2022, 3:50 pm

Baadhi ya wananchi Wilayani Mpanda wamesema wivu wa mali, hofu ya kupoteza nafasi na kutozimudu hasira zimekuwa ni sababu za migogoro mingi ndani ya ndoa.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema ndoa nyingi zimekuwa zikikumbwa na migogoro ya mara kwa mara kutokana na wivu wa mali na kufanya maamuzi bila kufanya uchunguzi wa kujua ukweli wa jambo hilo.

Kwa upande wake mwanasaikolojia David amesema sababu ambazo zinaweza kupelekea migogoro ndani ya ndoa ni pamoja na malezi na jamii huku akishauri watu kupata huduma ya kisaikolojia wakiwa kwenye mahusiano na wakiwa ndani ya ndoa.

Migogoro kwenye mahusiano na ndani ya  ndoa imekithiri hivi karubuni huku matukio ya mauaji yakiongezeka kutokana na migogoro hiyo.