Mpanda FM

IGP SIRRO: POLICE FANYENI KAZI KWA UADILIFU

25 May 2022, 4:17 pm

Mafisa wa polisi mkoani katavi wametakiwa kufanya kazi kwa ubora huku wakizingatia nidham usiri na uadili katika kutoa huduma kwa wananchi.

hayo yameelezwa na kamanda wa jeshi la polisi nnchi IGP Simon Siro katika uzinduzi  wa zahanati ya polisi mkoani hapa huku akiwaasa wananchi kutoa taarifa pale  wasipopata huduma inayoridhisha katika zahanati hiyo.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa zahanati hiyo Mrakibu Msaidizi wa polisi mkoani hapa ASP Omari Selemani Mwenkali amesema  zaidi ya shilingi Milioni Mia Moja zimtumika katika zahanati hiyo.

kwa upande wake  mkuu wa wilaya ya mpanda Jamila Yusuph Kimaro amemuomba kamanda siro kumsea kwa rais samia kuwapatia watumishi katika vituo vipya  vya afya pamoja na vifaa tiba ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

nae kamnda wa jeshi  polisi mkoani hapa Ali Makame Hamadi amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye zahanati hiyo kupatiwa matibabu kwan huduma zinazotolewa haziangalii nafasi ya mtu katika jamiii.