Mpanda FM

MGANGA WA KIENYEJI MBARONI KWA ULAWITI

23 May 2022, 1:32 pm

 

Jeshi la polisi mkoani katavi limefanikiwa kumkamata mganga wa kienyeji akili abakuki almaarufu kama jimmy mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa majengo kwa tuhuma za kulawiti watoto wenye umri kati ya miaka 6 hadi 12 alipokuwa akiwapatia matibabu ya tiba asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Sylvester Ibrahim amesema  mganga huyo amekamatwa mei 8   mwaka huuu  baada ya mama mmoja  kusikia kutoka kwa watoto wake wakihadithiana namna mganga huyo alivyo wafanyia vitendo hivyo.

Mpanda radio fm imekutana na  mmoja   wa wazazi ambae mtoto wake wa tatu wamefanyiwa  vitendo hivyo na  kueleza kuwa  mganga huyo alikuwa akihimiza kulala na watoto hao  pamoja kwa madai ya kuwafanyia tiba za usiku  licha ya yeye kutofaham kilichokuwa kikiendelea.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kata ya makanyagio  athumani lubwe amekiri kumpokea mganga huyo mwezi wa sita mwaka 2021  akiwa anaitaji  kupewa makazi katika kata yake.

Afisa mahusiano hospital ya rufaa mkoani hapa Emanuel  tinda  amethibitisha kupokea watoto saba  ambapo kati yao wakike wakiwa  ni wa 3 na wakiume 4  huku akisema kuwa kwa watoto wa kiume imekuwa vigumu kutambulika kuafanyia vitendo hivyo kwa kuwa ni mda sasa tangu wafanyiwe viytendo vivyo.

Hata hivyo jeshi la polisi mkoani hapa  limetoa rai kwa wananchi kuendelea kuwa fichua  watu  wenye mienendo ama viashiria vya kihalifu  kwani matokeo vya vitendo hivyo  hukwamisha maendeleo ya jamiii nzima.