Joy FM

Baiskeli 27 zagawiwa kwa wakulima wawezeshaji wa zao la pamba

3 December 2024, 11:22

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akikabidhi baiskeli kwa wakulima wawezeshaji wa zao la pamba, Picha na Michael Mpunije

Mkuu wa Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isac Mwakisu amesema serikali itaendelea kuwasaidia wakulima kwa kuwawezesha nyenzo mbalimbali zitakazowawezesha kulima kilimo chenye tija.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Halmshauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma imekabidhi baiskeli 27 kwa wakulima wawezeshaji wa zao la Pamba ili zitumike kutembelea  na kuhamasisha wakulima  wa zao hilo kuongeza uzalishaji na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akikabidhi baiskeli kwa wakulima wawezeshaji wa zao la pamba, Picha na Michael Mpunije

Akikabidhi baiskeli hizo mkuu wa Wilaya ya Kasulu kanali Isaac mwakisu amewataka wakulima wawezeshaji na AMCOS mbalimbali zilizokabidhiwa baiskeli hizo zitumike katika kufikia  matarajio ya kutoa Elimu kwa wakulima wengi zaidi na  kuongeza bidii katika uzalishaji wa zao la Pamba wilayani  Kasulu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Michael Mpunije

Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Kasulu Bw.Michael kihiga amesema wanatarajia kufikia malengo ya uzalishaji wa zaidi ya kilo milioni 5 za pamba katika msimu huu wa kilimo licha ya msimu uliopita kushindwa kufikia malengo kutokana na mvua nyingi zilizoathiri uzalishaji wa zao hilo la Biashara.

Sauti ya Mkaguzi wa Pamba wilaya ya Kasulu Bw. Michael Kihiga

Kwa upande wake  Anna titus mwanandota mkulima mwezeshaji kata ya nyamyusi na  na Mariamu James mwenyekiti wa AMCOS mwitiri kata ya Asante Nyerere wamesema baiskeli hizo watazitunza na kuhakikisha wanafikia walengwa wote ili waweze kunufaika na kilimo cha pamba.

Sauti ya Anna titus mwanandota mkulima mwezeshaji kata ya nyamyusi na  na Mariamu James mwenyekiti wa AMCOS mwitiri kata ya Asante Nyerere.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akikabidhi baiskeli kwa wakulima wawezeshaji wa zao la pamba, Picha na Michael Mpunije