Askofu Mlola awataka vijana kukemea rushwa Kigoma
25 November 2024, 14:27
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola amewataka vijana kuwa mstari mbele kukemea vitendo vya rushwa kwenye jamii hasa kipindi hiki cha uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Na Emmanuel Kamangu
Vijana mkoani Kigoma wametakiwa kuhakikisha wanakemea ruswa na wajitahidi kuchagua viongozi ambao watakuwa dira ya maisha yao.
Wito huo umetolewa na Askofu wa Jimbo katoliki la Kigoma Muhashamu askofu Joseph Roman Mlola katika adhimisho la misa takatifu ambayo imefanyika katika Parokia teule ya Mtakatifu Maxmillian Maria Kolbe ikiwa ni sikukuu ya vijana wakatoliki Duniani na kuwahimiza vijana kuhakikisha wanachagua viongozi wasio wala rushwa na wenye ali ya kupiania maendeleo.
Aidha Askofu Mlola amewataka vijana kupenda neno la Mungu ili kuwapa uwezo wa kuishi kwa kufanya matendo mema na kuepuka kufanya maovu huku akiwataka zaidi kuwatunza wazazi na wazee ili kupata Baraka za Mungu.
Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao wametoka parokia mbali mbali za mkoa wa kigoma wakiwa wamejaa fura juu ya sherehe hii ya vijana wakatoliki Duniani wamesema wanawajibu mkubwa wa kuwa kielelezo katika jamii hasa kwa kusimama imara katika kusimamia maendeleo ya kanisa na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Vijana jimbo katoliki la kigoma wameadhimisha sherehe hii ya vijana wakatoliki Duniani kwa kufanya matendo ya huruma kwa kuwatunza vitu mbali mbali ikiwemo nguo , sabuni , mafuta ya kujipaka wafungwa katika gereza la kasulu , wagonjwa katika hospital ya mji kasulu wakiwemo watoto yatima wa centre of hope.