Sibuka FM

Ndaki akabidhi madawati 161 jimbo la Maswa magharibi

12 October 2026, 14:28

Mbunge wa jimbo la Maswa magharibi,Mashimba Ndaki (kushoto) akimkabidhi madawati 161 afisa elimu kata ya Busangi, Mwalimu Levina James Picha na Samwel Mwanga

“Tunahitaji sana miundombinu bora ya elimu ili kurahisisha mazingira ya ufundishaji kwa wanafunzi mashuleni ili kuongeza ufaulu pamoja na kuongeza uelewa zaidi”.

 Na,Daniel Manyanga 

Wadau mbalimbali wa masuala ya elimu wilayani Maswa mkoani Simiyu wameombwa kuendelea kujitokeza na kuchangia madawati kwa ajili ya wanafunzi waliopo kwenye shule mbalimbali za wilaya hiyo ili kuwawezesha kuwa na mazingira bora ya kujifunzia hali itakayo ongeza ufaulu zaidi.

Levina James na Angelina Julius ni maafisa elimu kata ya Busangi na Mwabayanda wametoa wito huo wakati wa hafla ya kupokea madawati 161 yaliyotolewa na mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki, ambapo wameeleza kuwa bado kuna uhitaji wa madawati mengine zaidi kutokana na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na shule za msingi na sekondari wilayani hapo.

Sauti ya afisa elimu kata ya Mwabayanda na Busangi

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Maisha Mtipa amezitaja jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa ajili ya wananchi kuchangia madawati, huku mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki akieleza kuwa bado inahitajika hamasa zaidi ili kuwawezesha wananchi kuona umuhimu wa kuchangia miundombinu ya elimu.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Maisha Mtipa na mbunge wa jimbo la Maswa magharibi,Mashimba Ndaki
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Maisha Mtipa (kushoto) akipokea madawati 161 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Maswa magharibi,Mashimba Ndaki Picha na Samwel Mwanga

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Maswa Dkt. Vicent Naano amesema kuwa serikali wilayani hapo itaendelea kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunzia wawapo shuleni ili kuongeza ufaulu.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt.Vicent Naano Anney