Sibuka FM

Wachimbaji wadogo wa madini tumieni mifumo rasmi ya kifedha

22 April 2026, 8:04 am

Pichani ni mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha akiwa katika kikao kazi Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Tumieni mifumo rasmi ya kifedha ili kuongeza thamani na kuweza kupata mikopo kwa urahisi kutokana na utunzaji wa kumbukumbu wa kifedha kwenye mifumo ya kidigitali na hii itatusaidia kujuwa kipato na matumizi katika shughuli zetu za uchimbaji wa madini”.

Na,Daniel Manyanga

Wachimbaji na wafanyabiashara wa madini mkoani Simiyu wameombwa kutumia mifumo rasmi ya kifedha kwa ajili ya uhakika wa usalama wa fedha zao, pamoja na kurahisisha ufuatiliaji wa maendeleo ya biashara zao jambo litakalowawezesha kutunza kumbukumbu za kifedha zitakazowasaidia kupata mikopo kwa urahisi kwenye taasisi mablimbali za kifedha na kuongeza mitaji yao.

Ushauri huo umetolewa na mchambuzi mwandamizi wa mifumo ya malipo kutoka benki kuu ya Tanzania (BOT) Robert Masalu wakati akizungumza na wachimbaji mbalimbali wa madini mkoani Simiyu, katika mafunzo ya masuala ya fedha yaliyofanyika mjini Bariadi mkoani Simiyu na kueleza kuwa ni muhimu wachimbaji hao wakatumia mifumo rasmi ya kifedha huku meneja wateja wakubwa wa bank ya KCB ,George Ngazi akiutaja mfumo wa kidigitali kama njia bora ya kuhifadhi kumbukumbu za kifedha. 

Sauti ya Robert Masalu na George Ngazi

Anamringi Macha ni mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa elimu kuendelea kutolewa kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini mkoni Simiyu juu ya matumizi ya mifumo rasmi ya kifedha.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Anamringi Macha

Mussa Kalidushi na Limi Silanga ni baadhi ya wachimbaji wa madini walioshiriki mafunzo hiyo ambao wameomba kuboreshewa mazingira ya kuzifikia taasisi za kifedha kwa urahisi na kuweza kuzitumia ikiwemo mashariti ya kupata mikopo nafuu yawe marahisi ili kuweza kukuza mitaji na uchumi wao.

Sauti ya wachimbaji wa madini