Sibuka FM

Shughuli za kibinadamu chanzo uharibifu wa mazingira Maswa

3 August 2023, 6:26 pm

Pichani:Mwenyekiti wa Asasi ya uhifadhi wa Mazingira Wilayani Maswa Issack Bwanga akiwa kwenye moja ya vitalu vya Miti.Picha na Alex Sayi.

Ongezeko la mifugo na ufugaji wa kienyeji,ukataji miti kwaajili ya ujenzi,kilimo,uchimbaji madini,kuni na mkaa umetajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.

Na,Alex Sayi.

Imebainishwa kuwa shughuli za kibinadamu zimeendelea kuchangia uharibifu wa mazingira Wilayani Maswa Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Radio Sibuka fm Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya utunzaji wa Mazingira Wilayani hapa,Bw,Issack Bwanga amesema kuwa kukauka kwa vyanzo vya maji ikiwemo mito na visima umesababishwa na ongezeko la shughuli za kibinadamu

Bwanga ameongeza kusema kuwa ongezeko la athali za mabadiliko ya tabia ya Nchi umechangiwa na jamii kuacha kusimamia kanuni za asili za uhifadhi wa Mazingira,huku mifugo ikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu huo wa mazingira.

Maria Chalya mwenye umri wa miaka(78) mwananchi na  mkazi wa Kata ya Sola Wilayani hapa akizungumzia suala la mabadiriko ya Tabia ya Nchi amewaomba wananchi kujenga tabia ya kupanda Miti ili waweze kushiriki utunzaji wa mazingira.

Pichani:Bi,Maria Chalya (78)mhifadhi wa mazingira akionyesha karatasi yenye kumbukumbu ya mwaka wake wa kuzaliwa.Picha na Alex Sayi.

Kwa upande wake Afisa Nyuki Wilaya ya Maswa Salumu kuzenza amesema kuwa Halmashauri  hiyo, katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi tayari imeanzisha Mradi wa kitalu cha Miti Kata ya Zanzui chenye thamani ya zaidi ya Sh.Mil 227.2,huku Halmashauri hiyo kwa ushirikiano na Wakala wa huduma za Mistu Tanzania(TFS)na Mamlaka ya bonde la Ziwa Victoria tayari wameshapanda Miti Elfu kumi kwa msimu wa mwaka 2019/2020.

“Mradi huu utasaidia utunzaji wa mazingira na vyanzo vya Maji kwa kuhifadhi maliasili,kupunguza kiwango cha gesi ukaa na kuongeza makazi ya viumbe hai”amesema Kuzenza.

Sanjari na hayo wakazi wilayani hapa wameendelea kuchukua tahadhali  kufuatia Mamla ya hali ya hewa Nchini(TMA) kutahadharisha uwepo wa  Mvua za El nino zinazo tarajiwa kunyesha Oktoba hadi Desemba Mwaka huu.