Sibuka FM

Rais atoa zana za kilimo Maswa kuongeza uzalishaji wa pamba

13 March 2024, 10:44 am

Picha ya ndege nyuki ni moja ya zana za kilimo zilizotolewa kwa ajili ya upuliziaji wa wadudu katika zao la pamba ili kuongeza tija katika zao hilo. Picha na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mh Aswege Kaminyoge   amemshukuru   Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zana za kilimo kwa wakulima wa kata  ya  Senani  ili kumsaidia  mkulima  katika  kuongeza  tija  katika  zao la pamba.

DC Kaminyoge  ametoa  shukrani  hizo  wakati  wa  kuzindua zana hizo za kilimo katika  kata  ya  Senani  na kuwataka wakulima kuongeza uzalishaji ili  kurudisha  fadhira  kwa  Rais aliyetoa zana  hizo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge

Kaminyoge amewataka wakulima kuzingatia kanuni  bora za kilimo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa zao  la pamba na kuweza  kujikwamua kiuchumi huku  akiwataka viongozi waliokabidhiwa kusimamia  ugawaji wa zana hizo bila upendeleo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge
Pichani mwenye kofia nyeupe ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Aswege Kaminyoge akizungumza na wananchi wa kata ya Senani katika uzinduzi wa zana za kilimo.

Ally  Mabrouk  ni mwakilishi  wa  Bodi  ya  Pamba  wilayani  Maswa  amesema  zana  hizo za kilimo  ni  kwa  ajili  ya wakulima kuwasaidia na vitatumika   bure hivyo mkulima  atahitaji  kwenda kujiandikisha, kukopeshwa na kwenda kutumia kisha kurudisha.

Sauti ya Ally Mabrouk Mwakilishi wa Bodi ya Pamba -Maswa

Akijibu swali la Jilala  Ngasa mkulima wa kata ya Senani kuhusu upimaji wa udongo upi unafaa kwa kilimo, Mkuu  wa  Divisheni  ya  Kilimo, Mifugo na  Uvuvi Robert  Urassa  amesema vifaa  vya  kupimia  udongo tayari vimewasili  na muda wowote zoezi  litaanza mara moja na wakulima watapimiwa udongo na kupata majibu pamoja na kupewa ushauri.

Sauti ya Robert Urasa Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Mifugo na Uvivu -Maswa

Baadhi ya wakulima wa kata  ya Senani ambapo mradi  huo wa  Jenga  Kesho iliyo Bora (BBT ) wamemshukuru  Rais kwa kuwaletea vifaa hivyo  vya kilimo kwani vitasaidia kuongeza uzalishaji wa  tija katika zao la pamba.

Sauti ya Baadhi ya Kulima Kata ya Senani wakitoa Shukurani zao

      

Ally Mabrouk kutoka Bodi ya Pamba akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya na Wananchi wa Senani kuhusu Upuliziaji kwa kutumia Ndege nyuki (Drons)