Sibuka FM

Mpango uboreshaji matumizi ya ardhi, milki kuondoa  migogoro ya ardhi Maswa

14 July 2023, 9:14 am

Mkurugenzi msaidizi wa mipango miji na vijiji kutoka wizara ya ardhi Imaculatha Senje akiongea na wadau wa ardhi Wilayani Maswa. Picha na Nicholaus Machunda

Uboreshaji  Usalama  wa  Milki  za  Ardhi  na  Mpango  wa  Matumizi  bora ya  Ardhi  Wilayani  Maswa, Mkoani  Simiyu  Utaenda  kuondoa  Changamoto  ya  Migogoro ya  Ardhi  kwa  Wananchi

Na Nicholaus Machunda

Imeelezwa  kuwa  Uboreshaji  Usalama  wa  Milki  za  Ardhi  na  Mpango  wa  Matumizi  ya  Ardhi  Wilayani  Maswa, Mkoani  Simiyu  Utaenda  kuondoa  Changamoto  ya  Migogoro ya  Ardhi  kwa  Wananchi.

Hayo yameelezwa  na  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mhe  Aswege  Kaminyoge  Wakati  wa  Mkutano  Mkuu  wa  Wadau  wa  Kujadili  Mpango  wa  Matumizi  bora  ya  Ardhi  uliofanyika  katika  Ukumbi  wa  Halmashauri   ya  Maswa.

sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge akiongea katika mkutano wa wadau wa ardhi

Imaculatha  Senje  ni  Mkurugenzi   Msaidizi  wa  Mipango  miji  na  Vijiji  kutoka  Wizara  ya  Ardhi  Nyumba na  Maendeleo  ya  Makazi  amesema  kuwa   Wizara  imekusudia  kupima vijiji  zaidi  ya  Mia  moja  na kutoa  Hati  Miliki  za  Kimila   Wilayani  Maswa  hali  itakayosaidia  kupunguza  kero  na Migogoro  inayotokana  na   matumizi  ya  Ardhi.

sauti ya Imaculatha Senje kutoka Wizara ya Ardhi

                  Insert  02  Imaculatha Senje –Wizara ya Ardhi

Wabunge  wa  Majimbo  ya  Maswa  Mashariki  na  Magharibi,   Mhe  Stanslaus  Nyongo  na  Mhe, Mashimba  Ndaki  wameipongeza  Serikali   ya  awamu  ya  sita  chini  ya  Mhe  Rais   Samia  kwakuleta  Mradi  huo  utaoenda  kuondoa  Migogoro  na  Mauaji  ya  ndugu  na  wana ukoo  wakigombania  Mipaka  ya  Ardhi.

sauti za Wabunge wa Maswa Stanslaus Nyongo na Mashimba Ndaki

Baadhi  ya  Wadau  walioshiriki  katika  Kujadili  mpango  huo  wa  Matumizi  Bora  ya   Ardhi  ni   viongozi  wa  Dini, Wazee  maarufu, Madiwani   na  viongozi wa  taasisi  mbalimbali  wakapata  nafasi  ya  kutoa  maoni  yao  kuhusu  mradi  huo  wa  Upimaji wa  ardhi  na  utoaji  wa  Hati  miliki  za  kimila.

sauti za baadhi ya wadau wa ardhi

Naye  afisa  Mipango  miji  mkuu  kutoka  Wizara  ya  Ardhi  Nyumba  na  Maendeleo  ya  Makazi  Aristides  Mulokozi  amesema  kuwa  mradi  huo  utagharimu zaidi ya  Shilingi  Bilioni  mia tatu na  arobaini  na  tano   kwa  Nchi  nzima  huku  Wilaya ya  maswa ikitarajia  kutumia  zaidi ya  Bilioni  tatu

sauti ya Aristides Mulokozi – afisa mipango mkuu wizara ya Ardhi