Wilaya ya Maswa yaja na mkakati wa uzalishaji zao la pamba msimu wa 2023/2024
9 September 2023, 6:50 pm
Na Nicholaus Machunda
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu imejipanga kuja na Mbinu na Mikakati itakayoongeza Uzalishaji wa zao la Pamba kwa Msimu ujao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndugu Maisha Mtipa wakati wa Mafunzo ya Kuwajengea Uelewa Madiwani wa Halmashauri ya Maswa kuhusu Kilimo cha zao la Pamba.
Akiwasilisha Mada juu ya Sheria zinazoongoza kilimo cha Pamba, Mwanasheria kutoka Bodi ya Pamba Tanzania Bi, Elizabeth Msuya amesema kuwa kwa Mjibu wa Kifungu cha Tano cha Sheria ya pamba, Bodi inajukumu la kuishauri Serikali juu ya kuleta Maendeleo katika Sekta ya Pamba.
INSERT 02. ELIZABETH MSUYA- MWANASHERIA WA BODI
Aggrey Mwanri ni Balozi wa Pamba Nchi Tanzania amesema kuwa ili kuwe na Tija katika Uzalishaji wa zao la Pamba ni vyema Wakulima wakaondokana na Kilimo cha Mazoea ambacho hakifuati kanuni kumi za Kilimo cha Zao hilo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilayani hapa Robert Urassa amesema kuwa kwa msimu wa 2023/ 2024 Wilaya ya Maswa inatarajia kulima Hekta zaidi ya Elfu Sitini na kuvuna Tani zaidi ya Elfu Sitini za Pamba huku akitaja mikakati ya kufikia malengo hayo.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wameahidi kushirikiana na Halmashauri katika kutoa Elimu kwa Wakulimu na wao Kuanzisha Mashamba Darasa yatakayokuwa mfano kwa Wakulima kwenda kujifunza.