Sibuka FM

Migogoro ya ardhi, mirathi yapatiwa mwarobaini Maswa

27 January 2024, 7:29 pm

Pichani mwenye suti ni mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe,Aswege Kaminyoge kulia kwake Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Maswa Mhe,Enos Missana na pili kulia kwake ni katibu tawala wilaya ya maswa Picha na Daniel Manyanga

Wananchi waitumie wiki na siku ya sheria kupata elimu ya kisheria ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima hasa migogoro ya ardhi na mirathi kwa sasa hairipotowi kwa wingi katika vyombo vya kutoa haki.”

Na,Daniel Manyanga

Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu Mhe,Aswege Kaminyoge amewaomba Wananchi wilayani hapo kuitumia wiki na siku ya sheria kupata elimu ya maswala ya kisheria ili  kumaliza migogoro ya ardhi na mirathi ambayo imeonekana kuwa mingi na kutishia amani kwa baadhi ya jamii.

Kaminyoge ametoa rai hiyo mapema leo hii akiwa katika viwanja vya stund ya zamani wakati wa ufunguzi wa wiki ya sheria ambapo amesema kuwa migogoro mingi inayoonekana kuripotiwa mara kwa mara  kwenye vyombo vya kutoa haki ni mogogoro ya ardhi na mirathi hivyo ni vyema sasa Wananchi kuitumia wiki hiyo kuelimishwa na hatimaye kuondokana na migogoro hiyo isiyo ya lazima.

Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe,Aswege Kaminyoge akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa wiki ya sheria

Kaminyoge ameongeza kuwa kuna migogoro mingine midogo midogo haipaswi hata kuripotiwa katika vyombo vya kisheria endapo wananchi wataitumia wiki ya sheria kupata elimu ya masuala ya kisheria ambayo itasaidikia kupunguza au kumaliza migogoro baadhi ambayo haihitaji usaidizi wa mahakama.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe,Kaminyoge akiwaomba wananchi kuitumia wiki ya sheria katika kumaliza migogoro isiyo ya lazima

Awali hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Maswa Mhe,Enos Missana amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya sheria hutumika kama jukwaa maalumu linalowakutanisha Mahakama na wadau wake muhimu ili kutoa elimu ya shughuli zitolewazo na mahakama na wadau wake walio katika munyororo wa utoaji haki.

Sauti ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Maswa Mhe,Enos Missana akieleza madhumuni ya wiki ya sheria nchini

Katika hatua nyingine Kaminyoge amemuagiza  Katibu tawala wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri wa wilaya ya maswa kuhakikisha wanashirikiana na Mahakama ya wilaya hiyo kuendelea kuelimisha wananchi  juu ya umuhimu wa wiki ya sheria ili waweze kujitokeza kwa wingi  siku ya kilele hicho  pamoja na wakuu wa idara mbalimbali kuweza kuhudhuria siku hiyo.

Uzinduzi wa wiki ya sheria umeenda sambamba na kaulimbiu isemayo ‘’Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa taifa Nafasi ya Mahakama na Wadau katika kuboresha mfumo Jumuishi wa haki Jinai”

Picha katika matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa wiki na siku ya sheria wilayani maswa uliofanyika stund ya zamani pich na Daniel Manyanga