Sibuka FM

Serengeti safari marathon kuunga mkono royal tour

13 November 2023, 9:24 am

Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon wakijiandikisha mara baada yakuhitimisha mbio zao.Picha na Alex Sayi

Mamia ya watanzania wajitokeza kushiriki mbio za Serengeti Safari Marathon kuunga mkono juhudi za Rais Samia za Royal Tour.

Na Alex Sayi

Mkuu wa wilaya ya Bunda mkoani Mara Vicent Naano amesema kuwa mbio za Serengeti Marathon zinaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia za Royol Tour na kuwataka watanzania wajenge tabia yakufanya utalii wa ndani.

Pichani:Kushoto mwenye Kofia aliyenyanyua mkono ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mkoani Mara Vicent Naano akiwaanda wakimbiaji wa mbio za km 5 kukimbia.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Mkuu wa Wilaya Bunda Vicent Naano

Afisa Mhifadhi Mkuu Agustin George Msesa msimamizi wa kitengo cha maendeleo ya Biashara(TANAPA)makao makuu amesema kuwa watanzania wanapaswa kushiriki utalii wa ndani kwenye hifadhi za Taifa ambazo zina kila kitu

Pichani:Afisa Mhifadhi Mkuu Agustin Msesa.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Afisa Mhifadhi Mkuu Agustin Msesa

Timothy Mdika Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon amesema kuwa kila mshiriki ambae hakupata Medani yake ya ushindi kwenye mashindano hayo atapata

Pichani:Timothy Mdika Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon
Sauti ya Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon Timothy Mdika

Nao baadhi ya washiriki wa mbio hizo Elizabeth Boniphace,Saimon Ngereja na Diani John wamezungumzia  faida na umuhimu wa mashindano hayo

Pichani:Baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon kushoto ni Diana John katikati Elizabeth Boniphace na kulia ni Saimon Ngereja:Picha na Alex Sayi
Sauti za baadhi ya washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon(Elizabeth Boniphace,Saimon Ngereja na Diana John